Hooza Media kufungua ofisi kuu nchini Tanzania
Kampuni ya Hooza Media imetangaza kufungua Ofisi ya Kanda nchini Tanzania ambapo inatarajiwa kurahisisha wateja nchini kupata huduma zake wakati muafaka.
Hooza Media imeanzishwa nchini Rwanda mwaka wa 2013.
Upanuzi wa huduma za Hooza Media ni sehemu ya mpango wa muda mrefu wa kampuni hiyo kufanya huduma za media na mawasiliano zipatikane kwa Waafrika wote bila kujali mipaka.
Hooza Media imeahidi kupiga hatua kuelekea huduma za haraka na za kisasa zaidi kuwafikia watu wengi katika Ukanda wa Afrika Mashariki na vile vile Afrika kama bara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hooza Media, Bwana Victor Nkindi anasema hii ndiyo njia inayowezekana ya kupanua shughuli katika eneo hili la Afrika.
Anaelezea kuwa kampuni hiyo kwa sasa ina mipango ya kupanua shughuli zake kwa nchi nyingi barani Afrika.
Hooza Media kwa sasa ina huduma nyingine katika nchi kama Mali, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi, Senegal, Cameroon, Kenya, Uganda, Botswana, Tanzania, Guinea, Ivory Coast na Rwanda.